Sunday, 27 December 2015

WANANCHI WATOA YAO YA MOYONI KUHUSU JITIHADA ZA KUPAMBANA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU


Hatua zinazochukuliwa na serikali za kukabiliana na kipindu pindu ni nzuri lakini zitafanikiwa endapo zitatekelezwa na kuendelezwa na wananchi husika katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na wananchi mbali mbali wakati wakiongea na redio Fadeco katika kipindi  cha  HABA  NA  HABA ambacho  kilikuwa  kinahoji hatua  zinazochukuliwa  na  serikali  kukabiliana na ugonjwa wa kipindu pindu.

Mmoja wa wananchi hao Ponsian Kanyamuka kutoka Wilayani Kyerwa amesema mikakati ya serikali kuhusu kukabiliana na ugonjwa wa kipindu pindu zinapaswa kuzingatiwa na wananchi katika   maeneo yao na kuifanya kuwa endelevu.

Wamesema mpaka sasa hali usafi katika mazingira ya wananchi ni ya kuridhisha kutokana na kuwa tayari wamekwisha kupata elimu ya kutosha kutoka kwa viongozi na wamesisitiza kuwa zoezi hilo linapaswa kuwa endelevu kwa wananchi wakishirikiana na viongozi wao.

No comments:

Post a Comment